Jumanne 9 Juni 2026 - 02:40
Baraza Kuu la Hawza za latuma Ujumbe wa Rambirambi kufuatia kufariki Ayatullah al-Udhma Fayyadh

Hawza/ Baraza Kuu la Hawza limetoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa Mtukufu Ayatullah Muhammad Ishaq Fayyadh, mmoja wa Marajii wa Taqlid wa Najaf Ashraf.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa rambirambi wa Baraza Kuu la Hawza kufuatia kufariki kwa Mtukufu Ayatullah Fayyadh, mmoja wa Marajii wa Taqlid wa Najaf, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake Yeye tutarejea.

Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah as amesema:

"Anapofariki Muumini mwanachuoni faqihi, hutokea pengo katika Uislamu ambalo hakuna kitu chochote kinachoweza kuliziba."

Kufariki kwa faqihi mtukufu na Marjii mwenye cheo kikubwa wa Hawza tukufu ya Najaf Ashraf, Mtukufu Ayatullah al-Udhma Hajj Sheikh Muhammad Ishaq Fayyadh (Mwenyezi Mungu aitakase nafsi yake tukufu), kumesababisha huzuni na masikitiko makubwa.

Mwanachuoni huyo mtukufu alikuwa miongoni mwa shakhsia mashuhuri zaidi wa hawza ya kielimu ya Najaf Ashraf, ambaye licha ya hatari zote na mashinikizo yaliyokuwa yakiitawala Iraq katika kipindi cha utawala dhalimu wa Baath, alibaki imara Najaf Ashraf na hakuwahi kamwe kuiacha ngome hiyo tukufu. Aliyatumia maisha yake yenye baraka katika kueneza mafundisho ya Qur’ani Tukufu, kusambaza utamaduni wa Ahlul-Bayt wa Isma na Twahara (as), kulea wanafunzi wenye elimu na ubora, kuhudumia Hawza, na kujibu mahitaji ya kidini na kiakili ya Umma wa Kiislamu, pia aliacha urithi mkubwa wa kazi za thamani katika fiqhi na elimu ya misingi ya sheria za Kiislamu.

Baraza Kuu la Hawza linatoa pole na rambirambi zake kwa hadhara takatifu ya Mtukufu Baqiyyatullah al-A’dham (roho zetu ziwe fidia kwake), Marajii wakubwa wa Taqlid na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (baraka zao zidumu), Hawza hususan Hawza tukufu ya Najaf Ashraf, wanafunzi na wapenzi wa marehemu huyo, pamoja na familia yake tukufu.

Baraza Kuu la Hawza

22 Dhul-Hijjah 1447 Hijria Qamaria.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha